Isaac Herzog amekosoa sera za Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu katika kukabiliana na vuguvugu la kususia bidhaa za Israel na kuonya kuwa utawala huo unakabiliwa na Intifadha ya kidiplomasia. Ameongeza kuwa Netanyahu ameshindwa kukabiliana na vuguvugu hilo. Radiamali kuhusiana na ususiaji wa bidhaa za utawala wa Kizayuni ulimwenguni zimeshadidi ndani ya utawala huo haramu baada ya shirika maarufu la mitandao ya mawasiliano la Ufaransa la Orange kutangaza kuwa litahatimisha ushirikiano wake na shirika la Partner la Israel kutokana na kushtadi mashinikizo ya kimataifa ya kususia bidhaa za utawala huo wa Kizayuni kwa sababu ya kuendelea kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina hususan kwa kuendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni. Vuguvugu la kususia bidhaa za utawala haramu wa Israel limepokelewa na kuungwa mkono kwa wingi katika miezi ya hivi karibuni na watu wengi katika nchi za Ulaya zikiwemo asasi za kujitegemea na za wanafunzi wa vyuo vikuu…/mh