Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, jopo la majaji wa kimataifa katika mashindano hayo walimtangaza mwakilishi wa Iran kuwa qarii au msomaji bora zaidi wa Qur'ani katika mashindano hayo.
Hii ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 9 iliyopita kwa mwakilishi wa Iran kusika nafasi ya kwanza katika mashindano hayo.
Nafasi ya pili imechukuliwa na mshiriki wa Malaysia na kufuatiwa na wawakilishi wa Ufilipino, Brunei na Algeria kwa taratibu.
Katika kitengo cha kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu au hifdhi, mshindi alikuwa mwakilishi wa Qatar na kufuatiwa na washiriki kutoka Kuwati na Tunisia kwa taratibu.
Sherehe za kufunga mashindano hayo zimefanyika Jumamosi usiku Juni 13, katika ukumbi wa Putra World Trade Center mjini Kuala Lumpur na kuhudhuriwa na mfalme wa Malaysia.
Mashindano ya 57 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Malaysia yalianza Jumanne wili iliyopita na kuendelea kwa siku tano kwa kuwaleta pamoja washiriki kutoka nchi 70.../mh