IQNA

Imam wa Yemen aliyepinga hujuma ya Saudia auawa

9:32 - June 21, 2015
Habari ID: 3316631
Magaidi wa kundi al Qaida wamemuua imam mmoja wa Yemen anayefahamika kwa kupinga mashambulizi ya umwagaji damu yaliyoanzishwa na Saudia katika ardhi ya Yemen mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu.

Vibaraka wawili wa al Qaida waliokuwa wamepanda pikipili jana walimuua Sheikh Abdu Bari al Aidarus, Imam wa msikiti katika wilaya ya Shibam katika mkoa wa Hadhramaut. Shirika rasmi la habari la Yemen (SABA) limeripoti kuwa Sheikh Abdu Bari alikuwa maarufu kwa kupinga mashambulizi ya umwagaji damu ya Saudia nchini humo. Utawala wa Aal Saud ulianzisha mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Yemen mwishoni mwa mwezi Machi bila ya kuidhinishwa na Umoja wa Mataifa, ikiwa ni katika juhudi za kuidhoofisha harakati ya wapiganaji wa Kihouthi ya Ansarullah na kumrejesha madarakani rais wa Yemen aliyejiuzulu Abd Rabbuh Mansour Hadi.Mansour Hadi anafahamika kama muitifaki mtiifu wa Saudi Arabia.../mh

3316577

captcha