IQNA

Utawala wa Kizayuni wa Israel wateka nyara meli ya Sweden ikielekea Ghaza

16:07 - June 29, 2015
Habari ID: 3321135
Wanamaji wa jeshi la utawala haramu wa Israel wameiteka nyara meli ya misaada ya Sweden iliyokuwa imebeba misaada ya Wapalestina walio katika eneo linalozingirwa la Ukanda wa Ghaza.

Meli hiyo iliyo iliyopewa jina la Marianne of Gothenberg, ilikuwa ikielekea kuvunja mzingiro wa Ghaza ikiwa katika msafara wa meli wa Uhuru 3 na  ilizingirwa na boti za jeshi la Israel Msafara huo unajumuisha meli nyingine tatu ambazo ni Rachel, Vittorio, na Juliano II ambazo sasa zimegeuka na kurejea zilikotoka kwa hofu ya kuhujumiwa na wanajeshi wa Israel.

Wanaharakati walio katika meli hizo wametoa wito kwa serikali zao kuhakikisha walio katika meli iliyotekwa nyara na Israel hawadhuriwi. Utawala wa Kizayuni umeiteka nyara meli hiyo katika hali ambayo mwezi Mei mwaka 2010 wanajeshi wa utawala huo waliishambulia meli ya wanarakati wa Uturuki ambayo ni moja ya meli za msafara wa Uhuru 1 kwenye pwani ya Ukanda wa Ghaza.

Kwa kushirikiana na Marekani, utawala wa Kizayuni umeliweka eneo la Ghaza chini ya mzingiro mkali wa kiuchumi kwa karibu miaka saba sasa na kusababisha mashaka na masaibu mbalimbali kwa raia wa Kipalestina wakazi wa eneo hilo ambao pia hukaguliwa na hujuma za kinyama za Israel.

3320443

captcha