Barzin Zarqami, katibu wa maonyesho hayo amesema baada ya kuendeleza shughuli zake kwa siku 20 kuanzia Julai 20, maonyesho hayo yatamalizika tarehe 27 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Maonyesho ya 23 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran yalianza mwanzoni mwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika Bustani ya Kujihami Kutakatifu mjini Tehran.
Maonyesho hayo hufanyika kila mwaka chini ya usimamizi wa Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa lengo la kustawisha na kuendeleza mafundisho na misingi ya Qur’ani Tukufu.../mh