IQNA

Shule mpya ya Qur'ani yafunguliwa Ghana

21:19 - August 20, 2015
Habari ID: 3349417
Shule ya Qur'ani na Sayansi za Qur'ani imefunguliwa nchini Ghana kwa hisani ya Taasisi ya Sheikh Eid ya Misaada ya Qatar.

Kwa mujibu wa gazeti la Al-Sharq, shule hiyo imeanzishwa kwa ushirikiano na wanachama Waqatari wa Kituo cha Kiislamu cha Abdullah ibn Khalifa.
Shule hiyo ina msikiti na kituo cha masomo ya msingi.
Kustawisha mafundisho ya Qur'ani Ghana, kuimarisha elimu ya kidini katika nchi hiyo ya Afrika na kulea kizazi cha vijana wenye ujuzi wa mafundisho ya Kiislamu ni kati ya malengo mapya ya shule hiyo mpya.
Kuna idadi kubwa ya wafuasi wa dini ya Kiislamu nchini Ghana ambapo Uislamu uliwasili karne ya 10 katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
Inakadiriw akuwa Waislamu ni takribani asilimia 20 ya wakaazi milioni 27 wa nchi hiyo.../mh

3345961

captcha