IQNA

Umoja wa Mataifa wakosoa wanazuoni Saudia waliotangaza vita dhidi ya Mashia

16:45 - October 14, 2015
Habari ID: 3385681
Umoja wa Mataifa umelaani hatua ya baadhi ya wanazuoni wa Saudi Arabia ya kutangaza kile walichotaja kuwa Jihad dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na Wakristo nchini Syria.

Adama Dieng, Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika masuala ya kuzuia mauaji ya halaiki na Jennifer Welsh, ambaye ni mshauri wa umoja huo katika masuala ya ulinzi wamesema matamshi hayo ya wasomi wa Kisaudi hayana msingi na ni ya kupotosha.

Maafisa hao wa UN wameongeza kuwa, kauli hiyo haitakuwa na tija nyingine ghairi ya kuzidi kuvuruga mambo na kushadidisha mapigano na umwagaji damu nchini Syria.

Wamesema kinachotakiwa sasa ni viongozi wa kidini katika eneo kusisitizia umuhimu wa kufanyika mazungumzo ya kuutafuitia ufumbuzi wa kudumu, mgogoro wa kisiasa unaozidi kutokota nchini humo.

Mgogoro wa Syria uliibuka tangu mwaka 2011, wakati makundi ya kigaidi yanayopata uungaji mkono wa silaha na fedha kutoka nchi za Magharibi, utawala wa Kizayuni wa Israel na baadhi ya nchi za Kiarabu, yalipoanzisha mashambulizi na hujuma za kila aina kwa lengo la kuiondoa madarakani serikali halali ya nchi hiyo, ya Rais Bashar al-Assad, njama ambazo hadi leo zimeambulia patupu.../

3385531

captcha