Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia imedai kuwa, watu hao wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine kwa upanga leo baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika katika operesheni za kigaidi.Hukumu ya kuuawa imetekelezwa leo katika kitongoji cha 12 nchini humo, imebainisha taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudi Arabia.
Sheikh Baqir al Nimr alikamatwa na kufungwa jela na utawala wa kifalme wa Saudia mwaka 2012 akiwa katika maandamano ya kupinga dhulma za utawala wa Saudia katika eneo la Qatif lenye idadi kubwa ya Waislamu wa madhehebu ya Shia. Mahakama Kuu ya Saudi Arabia ilikuwa imepasisha hukumu ya kifo iliyotolewa na mahakama moja ya nchi hiyo dhidi ya msomi huyo na utekelezaji wake ulikuwa ukisubiri saini ya Mfalme Salman bin Abdulaziz.
Sheikh Nimr Baqir al Nimr amekuwa akipigania uhuru na haki za binadamu hususan za Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaokandamizwa sana nchini Saudia.