IQNA

Rais Rouhani alaani kuuawa shahidi Sheikh Nimr

15:44 - January 03, 2016
Habari ID: 3470011
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hatua iliyochukuliwa na Saudi Arabia katika kumuua shahidi ni dhidi ya Uislamu na ubinadamu na kwamba kitendo hicho kimefanyika katika fremu kuibua hitilafuna kuchochea ugaidi na misimamo mikali.

Katika ujumbe uliotolewa siku ya Jumamosi kufuatia kuuawa shahidi Sheikh Nimr Baqir Nimr, mwanazuoni mtajika wa Kiislamu Saudia. Huku akilaani kitendo hicho cha utawala wa Aal Saud, Rais Rouhani ameongeza hakuna shaka kuwa kitendo hicho cha serikali ya Saudi Arabia kitapelekea utawala huo kuchukiwa zaidi duniani hasa katika nchi za Kiislamu.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kitendo hicho cha Saudia Arabia cha kumuua Sheikh Nimr pia kitachangia katika kuvuruga uthabiti wa eneo, kuibua vita na machafuko.
Rais Rouhani katika ujumbe huo amesema, hata kama Waislamu nchni Iran wanajiunga na Waislamu kote duniani katika kulaani kitendo hicho kilicho dhidi ya ubinadamu, lakini hawataruhusi jinai hii itumiwe na baadhi ya watu kuchukua hatua za kuvunja sheria na kuvunja hadhi ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Ikumbukwe kuwa siku yua Jumamosi, Wizara ya Mambo ya Ndani Saudi Arabia ilitangaza kuwa Sheikh Nimr Baqir Al Nimr mwanazuoni maarufu wa Kiislamu na mtetezi wa haki za binadmau ameuawa kufuatia amri ya mahakama. Jinai hiyo imelaaniwa vikali na viongozi, shakhsia wa kisiasa na kidni kote duniani.

3464155

captcha