Waziri Mkuu Yahya Ould Hademine alitoa tangazo hilo na kuongeza kuwa, shule 16 mpya za Qur'ani zitaanzishwa maeneo mbali mbali ya nchi hiyo.
Aidha aliongeza kuwa kituo cha kieneo kitaanzishwa kwa ushirikiano na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (ISESCO) la Jumuiya ya Ushirikiano wa nchi za Kiislamu OIC ili kustawisha elimu ya msingi nchini humo.
Hademine alibainisha kuwa serikali ya Mauritania ikishirkiano na Banki ya Maendeleoya Kiislamu inapanga kufadhili shule za Qur'ani nchini humo.
Uamuzi huo umekuja baada ya jumuiya Kiislamu Mauritania kuitaka serikali kufungua tena shule na taasisi za Qur'ani zilizofungwa nchini humo.
Ikumbukwe kuwa Desemba mwaka jana, kulifanyika maandamano maeneo kadhaa ya Mauritania kulaani hatua ya serikali kufunga vituo kadhaa vya Qur’ani na chekechea.
Viongozi wa kidini na wahubiri nchini humo nao pia wameonya kuhusu kuvurugwa masomo ya kidini na Qur’ani nchini humo.
Mauritania ni nchi ya eneo la Maghreb huko magharibi mwa Afrika Kaskazini na inakadiriwa kuwa na idadi ya watu milioni 4 ambao karibu wote ni Waislamu.