Sherehe hizo zilifanyika katika mji wa Constantine kaskazini mashariki mwa Algeria na kuhudhuriwa na waziri wa Awqaf na masuala ya kidini nchini humo.
Washiriki katika hafla hiyo wametoa wito kuanzishwa zawadi itakayopewa jina za la ‘Nishani ya Mhududumu wa Qur’ani’ kwa lengo la kuhimiza harakati zenye lengo la kuutetea Uislamu mkabala wa vitendo vya kuivunjia heshima dini hii tukufu.
Wiki ya Qur’ani mwaka huu nchini Algeria imefanyika kwa nara ya ‘Kazi: Thamani Katika Mafundisho ya Qur’ani’ ambapo kulikuwa na washiriki wa matabaka mbalimbali wakiwemo wanazuoni wa kidini na wasomi wa Qur’ani.