Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, tukio hilo limejiri Ijumaa tarehe 8 Januari katika mji wa Sekondi-Takoradi magharibi mwa Ghana.
Raia mmoja wa Ghana na watu wengine wawili wenye asili ya Lebanon walikuwa wakiishi katika nyumba hiyo ambayo wakati wa kuteketea hapakuwa na mtu yeyote ndani.
Baada ya moto huo mkubwa kuzimwa, wazima mota walibaini kuwa kila kitu kilikuwa kimeteketea isipokuwa nakala ya Qur’ani ambayo haikuguswa na moto hata kidogo.
Kwa mara kadhaa sasa katika maeneo mengi duniani kumeripotiwa kuteketea nyumba lakini nakala za Qur’ani zikawa hazijaguswa na moto hata kidogo.