IQNA

Zarif: Saudia inachochea uhasama katika eneo

9:16 - January 12, 2016
Habari ID: 3470033
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa stratijia ya Saudi Arabia ni kutoa pigo dhidi ya makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1 na kuzidisha mivutano ya kimadhehebu katika eneo al Mashariki ya Kati.

Dakta Muhammad Javad Zarif amesema katika makala yake iliyochapishwa kwenye gazeti la New York Times la Marekani kwamba: Inasikitisha kuona baadhi ya nchi zikifanya njama za kukwaza mchakato wa Iran wa kutaka kuamiliana vyema na nchi mbalimbali duniani na baada ya kufikiwa makubaliano ya muda ya nyuklia Novemba mwaka 2013, Saudi Arabia ilitumia rasilimali na nguvu zake zote kwa ajili ya kufelisha mapatano hayo.

Zarif ameongeza kuwa, hii leo pia baadhi ya viongozi wa serikali ya Riyadh si tu kwamba wanazuia kurejeshwa hali ya kawaida bali wanafanja njama za kuliburuta eneo la Mashariki ya Kati katika mapigano.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema ushenzi unadhihiri vyema kwa sasa nchini Saudia ambako katika siku moja tu walikatwa vichwa watu 47 akiwemo mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu, Sheikh Nimr Baqir Nimr ambaye amesabilia maisha yake yote kwa ajili ya kukabiliana na ukatili na kutetea haki za raia.

Javad Zarif amesema uvamizi wa Saudia nchini Yemen na uungaji mkono wa Riyadh kwa makundi ya kigaidi vinaonekana wazi mbele ya watu wote lakini fitina za utawala huo dhidi ya Iran zimefeli kutokana na subira ya Tehran katika jamii ya kimataifa.

http://iqna.ir/fa/news/3466472

captcha