
Kwa mujibu wa tovuti ya Al-Maghribia, awamu hii ya mashindano imeandaliwa na Jumuiya ya Badirah ya Uhusiano wa Kijamii na Maendeleo.
Jopo la majaji katika tamasha hilo wanaongozwa na Ustadh Hajar Boussak, qarii mtajika wa Morocco ambaye alikuwa mshindi wa Tamasha la Kwanza la Tajweed ya Qur'ani nchini humo.
Sheikh Saeed Muslim ambaye aliongoza jopo la majaji katika tamasha la pili, pamoja na maqarii wengine mashuhuri wako katika jopo la majaji wa tamasha la mwaka huu.
Tamasha hilo ambalo linamalizika leo baada ya kuanza tarehe 29 Janari limehudhuriwa na maqarii 400 kutoka maeneo mbali mbali ya Morocco na nchi kadhaa za Kiarabu na Kiislamu.
Kuna washiriki kutoka makundi kadhaa ya umri na mshindi katika kila kundi atatunukiwa zawadi.
Allamah Muhammad al-Qantawi, qarii mashuhuri wa Morocco ambaye pia ametoa mafunzo kwa maqarii bingwa nchini humo anatazamiwa kuenziwa katika tamasha hilo.