IQNA

Waislamu nchini Marekani

Trump amepelekea kungozeka chuki dhidi ya Uislamu

14:44 - March 12, 2016
Habari ID: 3470193
Waislamu nchini Marekani, wamesema kuwa maneno ya chuki dhidi ya dini tukufu ya Kiislamu yanayotolewa na viongozi wa chama cha Republican, ndiyo sababu ya kuongezeka hujuma na mashambulizi dhidi ya Waislamu nchini humo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Taarifa iliyotolewa Alkhamisi na viongozi wa jumuiya za Waislamu nchini Marekani mbele ya waandishi wa habari mjini Washington imemtaka Donal Trump, anayewania kuteuliwa na chama cha Republican kugombea urais nchini Marekani, kuwaomba radhi Waislamu kutokana na matamshi yake ya Jumatano yaliyojaa chuki dhidi yao. Wakati akizungumza na kanali ya televisheni ya CNN, Trump alisema kuwa Uislamu unachafua sura ya Marekani. Nihad Awad, Mkurugenzi wa Baraza la Mahusiano la Kiislamu nchini Marekani CAIR, amesema kuwa, Trump lazima awaombe radhi Waislamu ambao baadhi yao wanahudumu jeshini, kama ambavyo pia kuna madaktari Waislamu wanaookoa maisha ya mamilioni ya Wamarekani na pia kuna maafisa wa ngazi tofauti serikalini wanaowahudumia raia. Aidha amesisitiza kuwa, mgombea huyo wa nafasi ya urais kwa tiketi ya chama cha Republican anatakiwa kuwaomba radhi wanawake Waislamu ambao kutokana na kuvaa kwao vazi la Kiislamu la hijabu, wananyanyasika na kutengwa katika idara za serikali na mashuleni nchini Marekani. Kabla ya hapo pia jumuiya za Kiislamu nchini Marekani zilikuwa zimetahadharisha kwamba, matamshi ya kichochezi ya Donald Trump, yanawaweka hatarini Waislamu nchini humo.
Trump aliwahi pia kusema kuwa Waislamu wanapaswa kuzuiwa kuingia nchini Marekani, matamshi ambayo yalikosloewa kote duniani.
/3482514 
captcha