Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Hujjjatul Islam wal Muslimin Abbas Muutaqidi Mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa (SAW) cha Iran akiwa ameamandamana na Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Senegal, hivi karibuni walifika katika Kanisa Kubwa (Cathedral) la mji mkuu wa nchi hiyo Dakar kwa ajili ya shughuli hiyo. Wakiwa hapo walimpa salamu za mwaka mpya wa Milladia Askofu Mkuu wa Dakar Benjamin Ndiaye na kumzawadia nakala ya Qur’ani Tukufu iliyotarjumiwa kwa Kifaransa.
Katika kikao hicho, Askofu Mkuu Ndiaye aliukaribisha kwa moyo mkunjufu ujumbe huo wa Iran na kubainisha furaha yake kuhusu mkutano huo.
Senegal ni nchi ya Afrika ya Magharibi upande wa kusini wa mto Senegal. Imepakana na Mauritania upande wa kaskazini, Mali upande wa mashariki, Guinea na Guinea-Bisau kwenye kusini na Bahari Atlantiki upande wa magharibi. Nchi ya Gambia iko ndani ya eneo la Senegal. Visiwa vya Cabo Verde viko 560 km mbele ya pwani la Senegal. Ilikuwa koloni ya Ufaransa hadi 1960. Asilimia 95 ya wakaazi wake ni Waislamu huku takribani asilimia tano wakiwa ni Wakristo Wakatoliki