IQNA

Tahadhari kuhusu kuenea Uwahhabi Misri

17:52 - April 11, 2016
Habari ID: 3470240
Mwanazuoni mwandamizi wa Kiislamu Misri ameonya kuwa itikadi potovu ya Uwahhabi inaenea Misri na hivyo kuhatarisha Uislamu wa wastani nchini humo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Sheikh Ahmad Karima ameiambia tovuti ya Ray al Yawm kuwa Mawahhabi wanaeneza itikadi zao za misimamo mikali katika nchi hiyo ya Kiarabu. Uwahabi ni itikadi potovu iliyobuniwa na Muhammad ibn Abdul Wahhab karne ya 17 Miladia nchini Saudia. Itikadi hiyo imepelekea kuibuka misimamo mikali ya kidini na makundi ya kigaidi kama vile Al Qaeda, ISIS au Daesh, Boko Haram na Al Shabab.

Sheikh Karima alikosoa sera za serikali za Misri kuhusu Uwahhabi na kusema sera hizo zimechangia kuenea itikadi hiyo potovu nchini humo. Katika miaka ya hivi karibuni, makundi yenye misimamo mikali yamekuwa yakiendeleza harakati nchini Misri. Katika miezi ya hivi karibuni makundi ya magaidi wa Kiwahhabi wamekuwa wakitekeleza hujuma na mauaji nchini humo.

Misri imekuwa ikikumbwa na misukosuko na ghasia tokea kuondolewa madarakani rais wa kwanza kuchaguliwa kwa njia ya demokrasia nchini humo, Muhammad Morsi mnamo Julai 2013 katika mapinduzi ya kijeshi yaliyochochewa na Rais Abdel Fattah al Sisi ambaye wakati huo alikuwa mkuu wa jeshi.

3487045

Kishikizo: misri uwahhabi iqna
captcha