Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Sheikh Abdulaziz Aal Sheikh, Mufti Mkuu
wa Saudia, sherehe za Maulid ya Mtume Muhammad SAW ni sherehe zisizo na
msingi wa kidini. Aidha amedai kuwa sherehe hizo ni potofu na ni
shirki huku akiwaonya wanaoshiriki katika Maulid ya Mtume Mtukufu SAW.Lakini katika upande wa pili, sambamba na maadhimisho ya kunyakua madaraka ukoo wa Aal Saud katika ardhi ya Hijaz ambayo iliadilishwa jina na kuwa Saudi Arabia, Mufti huyo amegeuka daraja 180 na kutoa fatwa mpya ya kuwalazimisha wananchi kusherehekehea siku hiyo. Sheikjh Abdul Aziz Aal Sheikh amebadilisha jina la Siku ya Kitaifa na kuitaja kuwa 'Siku ya Kushukuru' na kusema ni wajibu wa kidini kuisherehekea.
Maulamaa wa Kiwahhabi wanawakera Waislamu waliowengi kwa misimamo yao ya kufurutu adha ya kuharamisha Maulid ya Bwana Mtume SAW.
Magaidi wakufurishaji wanafuata itikadi za Kiwahhabi wamekuwa wakitekeleza mauaji dhidi ya Waislamu wanaoshiriki katika Maulid ya Mtume SAW.
