IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Qur’ani ya Port Said: Washindi wa Raundi ya Kwanza Watajwa

20:57 - February 06, 2024
Habari ID: 3478314
IQNA - Jopo la waamuzi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani yanayoendelea Port Said, Misri, limewataja washindi wa duru ya kwanza.

Awamu ya 7 ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Port Said ilianza siku ya Ijumaa.

Washiriki wanashindana katika kategoria za kuhifadhi Qur'ani, qiraa, Ibtihal, na kuhifadhi Qur'ani kwa watoto.

Baada ya kumalizika kwa duru ya kwanza na tathmini zilizofanywa na wajumbe wa jopo, washiriki 24 walichaguliwa kushindana katika hatua inayofuata.

Kutoka kati yao, 12 wataingia kwenye mzunguko wa mwisho, kulingana na waandaaji.

Qari mashuhuri, wataalamu na wanaharakati wa Quran kama Sheikh Abdul Fattah al-Taruti, Abdul Karim Salih, Muhammad Fathullah Bibris, na Hisam Saqar ni wajumbe wa jopo la wasuluhishi.

Toleo la mwaka huu limepewa jina la qari maarufu wa Misri Sheikh Shahat Muhammad Anwar (1950-2008).

Port Said Int’l Quran Contest: Winners of First Round Named  

3487094

captcha