Mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu yanafanyika nchini Gambia kwa kuhudhuriwa na wawakilishi wa nchi 28.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, gazeti la The Guardian limeandika kuwa, hayo yaliyoanza Jumanne wiki hii kwa anwani ya kumbukumbu
za mwaka wa 22 wa mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 1994 nchini humo
yanatambuliwa na serikali ya Banjul kama mapinduzi ya kitaifa. Waandaaji
wa mashindano hayo wamewashajiisha Waislamu kusoma na kufahamu
mafundisho adhimu ya kitabu hicho cha mbinguni na kwamba kutalii na
kufahamu Qur'ani kutasaidia kutatua matatizo ambayo yanawakabili
Waislamu hii leo. Katika ufunguzi wa mashindano hayo, Fatou Lamin Faye, Waziri wa Elimu ya Msingi wa Gambia amesema kuwa,
vitendo vya watu wenye kufurutu ada na ugaidi vimesababisha dini ya
Uislamu na Waislamu kwa ujumla kutiliwa shaka kiasi kwamba hii leo kila
Mwislamu anafuatiliwa kwa kudhaniwa kuwa gaidi. Waziri wa Elimu ya
Msingi nchini Gambia ameongeza kuwa, mienendo ya magaidi hao wanaojiita
wafuasi wa Uislamu, imewasababishia Waislamu wa kweli changamoto nyingi
katika kutetea Uislamu.