IQNA

Hizbullah yaionya Israel kuhusu uchokozi huko Shab'a

13:52 - August 19, 2016
Habari ID: 3470531
Harakati ya mapambano ya Kiislamu (muqawama) ya Lebanon Hizbullah imeuonya vikali utawala wa Kizayuni wa Israel kufuatia uchokozi wake katika mashamba ya Shab'a.

Taarifa ya Hizbullah imeeleza kuwa uchokozi huo unaonyesha kuwa tamaa na uchu ulionao utawala wa Kizayuni kwa utajirina mamlaka ya kujitawala ya Lebanon hauna kikomo wala mpaka.

Kwa siku kadhaa sasa, utawala wa Kizayuni umekuwa ukiendeshamtawaliashughuli za ujenzi wa barabara katika eneo moja la mashamba ya Shab'a ya Lebanon unayoyakalia kwa mabavu.

Taarifa ya Hizbullah imeitaka serikali ya Lebanon itekeleze jkumu lake la kulinda mamlaka ya kujitawala na kuchukua hatua zinazohitajika kukabiliana na uchokozi huo usiokubalika wa utawala wa Kizayuni.

Mkuu wa majeshi ya Lebanon Jean Kahwagi alisema hapo jana kuwa vikosi vya jeshi vimejiweka tayari kukabiliana na utawala wa Kizayuni. Amesisitiza kuwa jeshi la nchi hiyo litakabiliana kwa uwezo wake wote lilionao na uchokozi wa Israel utakaoilenga Lebanon,

Kahwagi aidha ametaka utawala wa Kizayuni uheshimu azimio nambari 1701 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililowezesha kufikiwa usitishaji vita katika vita vya mwaka 2006 na ambalo linautaka utawala huo haramu uheshimu mamlaka ya kujitawala na ardhi yote ya Lebanon.

h3460739/

captcha