IQNA

Msomi bingwa katika Ulimwengu wa Kiislamu aaga dunia

16:04 - October 24, 2016
Habari ID: 3470633
IQNA-Ustadh Bashir Jazairi, msomi bingwa katika vyuo vikuu vya Iran, Iraq na Algeria ambaye pia alikuwa mtangazaji wa radio na televisheni ameaga dunia mjini Tehran akiwa na umri wa miaka 80 kufuatia mshutuko wa ubongo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kutokana na umahiri wake katika kutunga mashairi na kuyasoma, Ustadh Jazairi aliwahi kushiriki katika mahafali ya usomaji iliyohudhuriwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Kutokana na harakati zake za Kiislamu ambazo ziliepelekea ahukumiwe kunyongwa na utawala wa Kibaath wa Saddam wa Iraq, Ustadh Jazairi alifanikiwa kukimbia nchi hiyo na kupata hifadhi Iran mwanzoni mwa muongo wa 80.

Tokea wakati huo, aliishi nchini Iran kwa muda wa miaka 35 ambapo kutokana na sauti yake nzuri na kubobea katika taaluma za fasihi na historia ya Ulimwengu wa Kiarabu, alikuwa moja ya nguzo muhimu za Idhaa ya Kiarabu ya Radio Tehran. Aidha sauti yake ilitumika katika vipindi vingi vya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Marehemu Ustadh Bashir Jazairi ameandika, kuhariri na kufasiri vitabu vingi muhimu vya fasihi na kidini.

Marehemu Ustadh Jazairi amezikwa leo katika Makaburi ya Behesht Zahara (SA) kusini mwa Tehran.

3540411

captcha