IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, ametoa salamu za rambirambi kufuatia kufariki dunia Ayatullah Hashemi Rafsanjani.
Ofisi ya kuhifadhi na kusambaza turathi za Kiongozi Muadhamu imesambaza
barua iliyoandikwa na Ayatullah Ali Khamenei kufuatia tukio hilo chungu.
Katika barua hiyo Kiongozi Muadhamu sanjari na kuonyesha masikitiko
yake makubwa kufuatia msiba huo, ametoa mkono wa pole kwa familia na
watu wa karibu wa mwanazuoni huyo, mwanamapambano, alimu na mfuasi wa
njia ya Imam Khomein (MA). Amesema na hapa ninamnukuu:
"Kumkosa Ayatullah Ali Akbar Hashemi Rafsanjani simtambui mtu mwingine
mwenye tajriba shirikishi na katika kipindi hiki kirefu nilichokuwa naye
nitamkumbuka hasa katika kipindi cha milima na mabonde ya kihistoria.