IQNA

Mahakama ya Nigeria yapinga amri ya marufuku ya Hijabu Shuleni

21:12 - February 08, 2017
Habari ID: 3470840
IQNA: Mahakama ya Rufaa katika jimbo la Lagos nchini Nigeria imetoa hujumu ya kupinga amri ya serikali ya jimbo hilo kupiga marufuku vazi la Hijabu kuvaliwa na washichana Waislamu shuleni.

Katika kikao chake cha Juanne, Mahakama ya ilitupilia mbali ombi la Serikali ya Jimbo la Lagos iliyotaka wasichana Waislamu wapigwe marufuku kuvaa Hijabu shuleni.

Serikali ya jimbo hilo ilitaka hijabu ipigwe marufuku katika shule za msingi na sekondari katika Jimbo la Lagos hadi pale Mahakama ya Juu Zaidi (Supreme Court) itakapotoa uamuzi kuhusu kesi hiyo.

Baada ya kusikiliza hoja za pande mbili, Jaji Muhammad Garba alitupilia mbali ombi la serikali na hivyo kuwarushusu wasichana Waislamu kuvaa Hijabu pasina kusumbuliwa hadi Mahakama ya Juu Zaidi itoe uamuzi wa mwisho.

Hukumu hiyo imepongezwa na Jumuiya ya Wanafunzi Waislamu Nigeria, MSSN, katika Jimbo la Lagos, Shaheed Ashafa, ambaye amesema walitarajia uamuzi hama huo.

Hukumu tarajiwa ya Mahakama ya Juu Zaidi kuhusu mvutano huo wa Hijabu inatazmaiwa kuwa na taathira kubwa miongoni mwa jamii ya Waislamu nchini Nigeria.

Mapema mwaka jana, jumuiya za Kaislamu nchini Nigeria zilitoa taarifa ya kulaani vikali azma ya Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo ya kutaka kupiga marufuku vazi la hijabu na kusema kuwa, sera kama hiyo ni njia ya kukwepa utatuzi wa matatizo ya kimsingi ya nchi hiyo. Aidha Jumuiya ya Mawakili Nigeria (NBA) ilisema kupigwa marufuku vazi la kujisitiri wanawake Waislamu yaani hijabu ni kinyume cha katiba ya nchi hiyo.

Kauli hizo zilitolewa baada ya Buhari kusema kuwa baadhi ya magaidi wa Boko Haram wanaotekeleza hujuma za kigaidi nchini ni wanawake wanaovaa hijabu na kwamba iwapo italazimu, serikali yake haitakuawa na njia nyingine ghairi ya kuchagua moja kati ya mambo mawili ima vazi la hilo la staha au usalama wa taifa.

3572370/

captcha