IQNA

Qatar yakosoa Saudia, UAE, Bahrain na Misri kwa kukata uhusiano

11:59 - June 05, 2017
Habari ID: 3471008
TEHRAN (IQNA) Baada ya Saudi Arabia, Misri, Imarati na Bahrain kukatika uhusiano na Qatar, wizara ya mambo ya nje wa Qatar imekosoa hatua hiyo.

Televisheni ya Al Alam imenukulu taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar ikisema hatua hiyo ya kukat uhusiano ni ya kusikitisha, haiwezi kutetewa na imechukuliwa kwa kutegemea madai ya urongo na yasiyo na msingi.

Taarifa hiyo imesema hatua hiyo ya kukata uhusiano haitakuwa na taathira katika maisha ya raia wa nchi hizo nne nchini Qatar.

Aidha Qatar imesema itachukua hatua za kukabiliana na njama zenye lengo la kuathiri vibaya uchumi wa watu wa nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi.

Mapema leo Nchi za Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu yaani Imarati, Bahrain na Misri zimekata uhusiano wao wa kidiplomasia na mahusiano yote wa majini na angani na Qatar zikiituhumu nchi hiyo kuwa inaunga mkono ugaidi na kuingilia masuala ya ndani ya nchi hizo.

Nchi ya kwanza kabisa kukata uhusiano wake na Qatar ni Saudi Arabia ambapo mapema leo asubuhi imetangaza kukata uhusiano wake na Doha na kusema "tunaziomba nchi zote ndugu zichukue hatua kama hii."

Baada ya tamko hilo, vibaraka wa Saudia yaani Bahrain, Imarati (UAE) na Misri nao pia wametangaza kukata uhusiano na Qatar.

3606530

captcha