IQNA

Gaidi ajaribu kumnyonga Mwanamke Mwislamu kwa hijabu aliyokuwa amevaa

11:44 - August 01, 2017
Habari ID: 3471095
TEHRAN (IQNA)-Mwanamke Mwislamu muuguzi katika eneo la Staffordshire Uingereza amehujumiwa na gaidi mwenye chuki dhidi ya Uislamu aliyejaribu kumnyonga bila mafanikio.

Gaidi huyo aliyetambuliwa kwa jina la Jake Hammersely, 25, alikamatwa alipomvua mwanamke muugizi Mwislamu hijabu yake na kuanza kumpiga makonde.

Taarifa zinasema gaidi huyo alimfunga muuguzi huyo hijabu yake shingoni na kumyonga. Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 29 alipojaribu kujitetea, gadi huyo alimpiga ngumu usoni na kumuacha na majeraha.

Baada ya Hammersley kukamatwa, alikiri kutekeleza hujuma zenye chuki za kidini, kutusi na kumpiga muuguzi mwislamu na kwa msingi huyo akahukumiwa kifungo cha wiki 40 gerezani.

Mwishoni mwa mwaka uliopita,Kamisheni ya Kiislamu ya Haki za Binadamu yenye makao yake mjini London iliandaamkutano wa kujadili suala lauenezaji chuki dhidi ya Uislamu, ubaguzi wa rangi na vilevile sababu ya kuongezeka chuki na hofu juu ya Uislamu katika Ulimwengu wa Magharibi.

Katika miaka ya karibuni, mbali na Uingereza, chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu na mashambulio ya mitaani dhidi ya Waislamu yameongezeka mnokatika nchi zingine za Ulaya.

3463527

captcha