IQNA

Uislamu unaenea kwa kasi Nepal, nchi ya Wahindu

11:33 - September 05, 2017
Habari ID: 3471159
TEHRAN (IQNA)-Uislamu unaenea kwa kasi sana Nepal, nchi ambayo aghalabu ya wakaazi wake wengi ni Wahindi au Mabaniani.

Kwa mujibu wa Khorshid Alam, Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu Nepal, idadi ya Waislamu nchini humo imekuwa ikiongezeka kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni.

Ameongeza kuwa, katika kipindi cha miaka 15 iliyopita, watu 100,000 wamesilimu katika nchi hiyo ya Asia. Alam ameendelea kusema kuwa idaid ya wanaokumbatia Uislamu inatazamiwa kuongezeka katika miaka ya hivi karibuni.

Hii ni katika hali ambayo watu wanaoacha Uhindu na Ubuddha na kuukumbatia Uislamu wanakabiliwa na changamoto nyingi na matatizo maisha. Hii ni kwa sababu Mabuddha na Wahindu wenye misimamo mikali wanachukizwa sana kuona watu wakisilimu.

Pamoja na kuwepo matatizxo kwa wanaosilimu, Uislamu unazidi kuenea kwa kasi Nepal.

Nchi ya Nepal, ambayo mji wake mkuu ni Kathmandu, iko Asia ya Kusini kwenye milima ya Himalaya inayopakana na Uhindi na China. Mlima Everest ambao ni mlima mkubwa kuliko yote duniani uko Nepal.

Wakazi wengi (81.3%) hufuata dini ya Uhindu. Ubuddha una 9% wa wakazi, ukifuatwa na Uislamu (4.4%), Ukirati (3.1%), Ukristo (1.4%) na dini za jadi (0.4%).


3463836
captcha