Mashindanao hayo yamefadhiliwa na Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudi Arabia na yamekamilika leo 23 Desemba 2024.
Hafla hiyo imefanyika kwa ushirikiano na Tume ya Waislamu ya Nepal na chini ya usimamizi wa Ubalozi wa Saudi huko Kathmandu.
Mashindano hayo yalivutia zaidi ya washiriki 750, wakiwemo wanafunzi wa kiume na wa kike kutoka shule mbalimbali na vituo vya Kiislamu kote nchini Nepal.
Washiriki walishindana katika makundi manne, wakionyesha ujuzi wao wa kuhifadhi na kusoma Qur’ani. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, tukio hilo ni sehemu ya juhudi za Saudi Arabia za kuendeleza mafundisho ya Qur'ani Tukufu miongoni mwa vijana Waislamu duniani kote.
Mashindano ya kwanza, yaliyofanyika mapema mwaka wa 2024, yalishuhudia wahifadhi 350 wanaume na wanawake wakishindana katika kuhifadhi Qur’ani.
Nepal, nchi isiyo na bandari katika Asia Kusini, ina Waislamu wachache wanaojumuisha takriban asilimia 5 ya wakazi wake. Licha ya kuwa ni wachache, Uislamu umekuwa dini inayokuwa kwa kasi zaidi nchini humo, ambayo sasa inashika nafasi ya pili kwa idadi kubwa ya wafuasi.
3491166