IQNA

11:59 - December 11, 2017
News ID: 3471305
TEHRAN (IQNA)-Shirika la mavazi ya michezo la Nike limeanza kuuza 'Hijabu ya Wanamichezo' ambayo ni maalumu kwa wanamichezo wa kike Waislamu wanaotaka kujisitiri.

Mradi wa Nike wa kushona mtandio na vazi maalumu  kwa ajili ya wanamichezo Waislamu ulianza mwezi Machi kufuatia maombi kadhaa.

Vazi hilo la Hijabu lilianzakuuzwa mapema mwezi huu wa Disemba ambapo unakadiriwa kugharibu $35 na hata unaweza kununuliwa kupitia tovuti ya shirika hilo.

Shirika la Nike lilifanya utafiki kabla ya kushona mtandio na vazi maalumu kwani wanawake wengi Waislamu waliuokuwa wakivaa mitandio ya kawadia katika michezo walikuwa wakilalamika kuwa wanashindwa kutekeleza harakati za kimichezo kikamilifu.

Kwa mfano mnyanyua vyuma Bi.Amna al Haddad wa Umoja wa Falme za Kiarabu aliliambia shirika la Nike kuwa  mtandio wake ulikuwa haupitishi hewa vizuri na ulikuwa unadondoka mara kwa mara. Naye Bi.Ibtihaj Muhammad ambaye aliiwakilisha Marekani katika mchezo wa vitara al maarufu Fencing katika michezo ya Olimpiki amekuwa akilalamika kuwa wakati alipokuwa akivaa mtandio wa kawaida alikuwa na tatizo la kusikia na hivyo wakati mwingine alikuwa akipewa kadi na refa.

Pamoja na hayo, kuna baadhi ya wapinzani wa Hijabu wenye chuki dhidi ya Uislamu ambao wametangaza kupinga hatua hiyo ya Nike kushona vazi maalumu kwa ajili ya kuwahudumiwa wanawake wanamichezo Waislamu wakidai Uislamu eti sasa unaenea hadi katika viwanja vya michezo.

.Nike yatangaza kuanza kuuza 'Hijabu ya Wanamichezo

3671156

 

Tags: iqna ، nike ، wanamichezo ، waislamu ، Hijabu
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: