Nahodha na nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Palestina Suleiman al-Obeid, aliuawa shahidi katika shambulizi la kinyama la utawala wa kizayuni wa Israel wakati alipokuwa akisubiri msaada wa chakula huko Ghaza siku ya Jumatano.
Akizungumzia hatua ya Muungano wa Vyama vya Soka vya Ulaya UEFA ya kumuenzi Suleiman Al-Obeid, anayejulikana kama "Pele wa Palestina, Mohammad Salah mshambuliaji wa timu ya soka ya Liverpool ya Uingereza ameihutubu UEFA kwa kuhoji mnaweza kutuambia jinsi alivyokufa?
Wahusika wa UEFA hawkupatikana mara moja kutoa maoni kuhusiana na matamshi haya ya Salah.
Katika taarifa yake ya kumuenzi nyota huyo wa soka wa Palestina UEAFA ilisema, al-Obeid ni kipaji ambacho kilitoa matumaini kwa watoto wengi, hata katika nyakati za giza.
UEFA imeendelea kumuelezea al-Obeid katika taarifa yake: "Swala, Lulu Nyeusi, Henry wa Palestina, na Pele wa soka ya Palestina, zote hizo ni lakabu za nyota huyo aliyepitia kwenye viwanja vya kuchezea soka vya Palestina" .
Chama cha Soka cha Palestina (PFA) kimetangaza kuwa al-Obeid, aliyeuawa shahidi akiwa na umri wa miaka 41, ameacha kizuka na watoto wawili wa kiume na watatu wa kike.
3494193