IQNA

Washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qurani ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu

22:41 - April 29, 2018
Habari ID: 3471488
TEHRAN (IQNA)- Washindi wa Mashindano ya Sita ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Wanachuo Waislamu wametangazwa leo Jumapili.

Mashindano hayo yalianza Ijumaa katika mji mtakatifu wa Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran na leo majaji wamewatangaza washindi katika kategoria za kuhifadhi na kusoma Qur’ani.

Kwa mujibu wa jopo la majaji, hafidh wa Qur’ani kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mujtaba Fardfani ameibuka mshindi katika kategoria ya kuhifadhi Qur’ani akifuatiwa na Harun Mamadu kutoka Niger huku Mohammad Hamid Hana wa Indonesia akichukua nafasi ya tatu.

Katika kitengo cha qiraa pia Mahdi Gholam-Nejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amechukua nafasi ya kwanza akifuatiwa na Mohammad Ali Foroughi wa Afghanistan huku Ahmed Jamal Kamal al-Mansarawi wa Iraq akiwa wa tatu.

Washiriki 44 kutoka nchi 35 za mabara ya Asia, Afrika, na Ulaya wameshiriki katika mashindano hayo ya wanafunzi Waislamu wanaosoama katika vyuo vikuu.

Jumuiya ya Harakati za Qur'ani ya Wanaakademia wa Iran inayofungamana na Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti Iran (ACECR) imekuwa ikiandaa mashindano ya Qur’ani ya wanafunzi Waislamu wa vyuo vikuu baada ya kila miaka miwili tokea mwaka 2006 kwa lengo la kuimarisha umoja na ushirikiano baina ya wanafunzi Waislamu kote duniani sambamba na kustawisha kiwango cha harakati za Qur’ani katika vyuo vikuu.

3710322

captcha