IQNA

17:28 - November 10, 2018
News ID: 3471736
TEHRAN (IQNA)- Mfuko mkubwa zaidi wa Kiislamu wa mafao ya uzeeni umezinduliwa nchini Kenya na kupewa jina la Salih.

Mfuko huo wa Kiislamu wa malipo ya uzeeni utaendesha shughuli zake chini ya usimamizi wa Mfuko wa Mafao ya Uzeeni  wa Kaunti za Kenya  (CPF) ambapo Waislamu na hata wasiokuwa Waislamu wanaweza kujiunga.

Salih ni mfuko wa kwanza wa malipo ya uzeeni Kenya ambao unazingatia mfundisho ya Kiislamu baada ya Halmashauri ya Malipo ya Uzeeni Kenya (RBA) kuidhinisha uanzishwaji mfuko kama huo.

Mfuko wa Uzeeni wa Salih unalenga kuwavutia Waislamu ambao wanaendesha masuala yao ya kifedha kwa mujibu wa mfundisho ya Kiislamu. Wanazuoni wa Kiislamu watakuwa katika bodi ya mfuko huo ili kuhakikisha unazingatia mafundisho ya Kiislamu. Kinyume na mifuko migine ya pensheni au malipo ya uzeeni, mfuko wa uzeeni wenye kuzingatia mafundisho ya Kiislamu hauwekezi fedha za wanachama katika bidhaa au huduma haramu kama vile viwanda vya pombe, viwanda vya nyama ya nguruwe, kamari , benki zenye kutoza riba n.k.

Mkuu wa CPF Hosea Kili amesema wanachama wa Mfuko wa Malipo ya Uzeeni wa Salih wanaweza kuhamisha fedha zao kutoka mifuko mingine hadi katika mfuko huu mpya wa Kiislamu.

Kiongozi wa Waliowengi katika Bunge la Kenya Aden Duale ametoa wito kwa Waislamu kujiunga na mfuko huo ili waweze kujitosheleza katika uzeeni.

/3762561

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: