IQNA

Hamas: Mapambano ya Palestina yamevuruga mahesabu ya adui Mzayuni

15:18 - November 15, 2018
Habari ID: 3471742
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema: Mapambano (muqawama) ya Palestina yamevuruga mahesabu ya adui na kubadilisha mlingano wa nguvu.

Ismail Haniya ameeleza kwamba: "Kwa ushindi waliopata wapigania ukombozi, taifa la Palestina limefikia natija na kubainikiwa kwamba, mapambano ndio njia pekee ya kuufikia ukombozi wa Quds Tukufu na ardhi yote ya Palestina".

Amesema harakati za wapigania ukombozi kwa muda wa chini ya wiki moja tu zimeleta ushindi dhidi ya utawala ghasibu na kusambaratisha operesheni za kiusalama za utawala wa Kizayuni.

Haniya amesisitiza kuwa, mapambano yanaendelea kupanuka na kustawi; na taifa la Palestina linaunga mkono muqawama; na vikosi vya wanamapambano wa muqawama vimetoa jibu kwa utawala wa Kizayuni kulingana na jinai na uchokozi uliofanya.

Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas ameashiria kujiuzulu Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni, Avigdor Lieberman na kueleza kwamba, kwa kujiuzulu Lieberman umepatikana ushindi mkubwa wa kisiasa; na tangazo lake la kujiuzulu, maana yake hasa ni kutangaza kushindwa utawala huo ghasibu.

Stratijia ya harakati za mapambano ya Kiislamu za Palestina ambazo zimeulazimisha utawala wa Kizayuni wa Israel kusitisha vita katika eneo la Ukanda wa Gaza imezusha hitilafu kubwa ndani ya baraza la mawaziri la serikali ya utawala huo haramu kiasi kwamba, mtikisiko huo umemlazimisha Waziri wa Vita wa utawala huo kujiuzulu na kuiweka serikali bandia ya Israel katika ncha ya kusambaratika.

3467226

captcha