IQNA

10:16 - September 12, 2019
News ID: 3472127
TEHRAN (IQNA) – Waalimu wametimuliwa katika shule moja huko Montreal, Canada baada ya kusistiza kuendelea kuva vazi la staha la Kiislamu, Hijab.

Kwa mujibu wa taarifa, jimbo la Quebec nchini Canada limeanza kutekekeleza sheria ya kuwazuia wafanyakazi za umma kudhihirisha kile kinachotajwa kuwa ni nembo za kidini. Sheria hiyo inaonekana kuwalenga zaidi wanawake Waislamu baada ya Hijabu kutajwa kuwa 'nembo ya kidini.'

Taarifa zinasema mwalimu Mwislamu aliomba kazi katika shule ya msingi ya Montreal na akafahmishwa na baada ya ombi lake kukubaliwa, alipewa muhula wa siku 15 kuvua Hijabu la sivyo afutwe kazi.

Walimu wote wa kike Waislamu wanaovaa Hijabu katika jimbo la Quebec Canada sasa wanabaguliwa na wanakosa fursa za kazi kutokana na sheria hiyo ya kibaguzi.

Francois Legault Waziri Mkuu wa Quebec ambaye chama chake cha mrengo wa kulia kimeshinda katika uchaguzi mwaka jana ndiye aliyewasilisha muswada wa sheria ya kupiga marufuku walimu, maafisa wa polisi, majaji pamoja na wafanyakazi wengine wa sekta za umma kuvaa vazi lenye 'nembo ya kidini'.

Mwezi Oktoba mwaka 2017, bunge la kieneo la Quebec lilipiga kura 65-51 kuunga mkono sheria ya kuwapiga marufuku wanawake Waislamu kuvaa Hijabu yenye kufunika uso mzima maarufu kama niqab wakiwa wanatumia huduma za umma.

Baraza Kuu la Wanawake Waislamu Canada limesema sheria hiyo inawalenga wanawake Waislamu katika jimbo la Quebec kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Tayari kumefanyika maandamano kadhaa kupinga marufuku hiyo ya hijabu.

Jimbo la Quebec liko mashariki mwa Canada na aghalabu ya wakazi wake huzungumza Kifaransa na mji wake mkuu ni Montreal. 

3841525/

Name:
Email:
* Comment: