IQNA

16:35 - October 22, 2019
News ID: 3472183
TEHRAN (IQNA) – Wapalestina yametoa wito kwa jamii ya kimataifa ichukua hatua za kuulinda Msikiti wa Al Aqsa ulio katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

Wito huo umetolewa kufuatia ongezeko la vitendo vya walowezi wa Kizayuni kuuhujumu na kuuvunjia heshima msikiti huo wakiwa wanaungwa mkono na jeshi la utawala wa Israel.

Wiki iliyopita pekee, walowezi wa Kizayuni wapatao 5000 waliuhujumu Msikiti wa Al Aqsa na kutekeleza ibadha za Kiyhaudi ndani ya msikiti huo wakiwa wanalindwa na jeshi la Israel. Hatua hiyo ilikuwa na lengo lwa kuwaudhi Waislamu ambao huswali katika msikiti huo.

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa mipango ya adui Mzayuni ya kuugawa msikiti wa al Aqsa itagonga mwamba na kusisitiza kuwa wananchi wa Palestina hawataruhusu kutekelezwa mipango ya adui na kubadilishwa athari na nembo za mji wa Quds.

Ismail Hania amesisitiza kuwa kuna udharura wa kukabiliana kwa dhati na kwa ushujaa na mipango ya adui Mzayuni na kueleza kuwa: Matukio yanayojiri katika eneo kivyovyote vile hayawezi kulisahaulisha suala la Palestina kwa sababu Quds itaendelea kuwa kituo cha mapambano na makabiliano dhidi ya adui Mzayuni.

Hania ameongeza kusema kuwa, utawala wa Kizayuni inastafidi na matukio na vita vya ndani katika baadhi ya nchi za eneo hili ili kusogeza mbele na kutekeleza njama zake hatari dhidi ya msikiti wa al Aqsa; lakini wananchi wa Palestina wataendelea kuutetea na kuilinda Quds na matukufu ya Kiislamu.

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas aidha amezitolea wito pande tatu za Palestina, Kiarabu na Kimataifa kuchukua hatua za kukabiliana na mpango wa utawala wa Kizayuni wa kuuyahudisha msikiti wa al Aqsa. Hania amezitolea wito pia nchi na wapigania uhuru wote duniani kuususia utawala wa Kizayuni na kuutenga ili uache mipango yake michafu dhidi ya msikiti huo mtakatifu.

Utawala wa Kizayuni unatekeleza misingi mitatu mikuu ambayo ni kuugawa utumiaji wa Msikiti wa Al Aqsa kisehemu na kiwakati, kuchimba mashimo ya chini kwa chini na kandokando ya msikiti na kuyahudisha maeneo ya jirani na mahala hapo patakatifu.

Hii ni katika hali ambayo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limethibitisha tena kwamba msikiti mtukufu wa Al-Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu ni milki ya Wapalestina.

3469717/

Name:
Email:
* Comment: