IQNA

Darul Iftaa ya Misri yaharamisha maandishi ya Qur'ani kwa alfabeti za Kilatini

13:49 - September 20, 2021
Habari ID: 3474316
TEHRAN (IQNA) – Darul Iftaa ya Misri imetangaza marufuku ya kuandika aya za Qur'ani Tukufu kwa alfabeti za kilatini.

Katika taarifa ambayo imechapishwa katika gazeti la Al Watan, Darul Iftaa al Misriyyah, ambayo ni moja ya taasisi muhimu zaidi za kutoa Fatwa za Kiislamu duniani, imesema haijuzu kubadilisha maandishi ya alfabeti au herufi za Kiarabu za Qur'ani.

Hivi karibuni Mmisri mmoja alitayarisha mbinu mpya ya kusoma Qur'ani Tukufu kwa Kiarabu kwa kutegemea herufi za kilatini bila kuwa na haja ya kujua kusoma herufi za Kiarabu.

Ubunifu huo umeibua mijadala katika mitandao ya kijamii na hivyo Darul Iftaa imetoa Fatwa ya kupiga marufuku uandishi wa Qur'ani Tukufu kwa herufi za kilatini au herufi zisizo za Kiarabu.

Fatwa hiyo imesisitiza kuwa, "haijuzu kubadilisha maandishi ya Qur'ani na Maulamaa wana jukumu la kulinda mfumo wa hati za Qur'ani na wasiridhie mabadiliko."

3998708

 

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha