IQNA

8:19 - December 04, 2019
News ID: 3472255
TEHRAN (IQNA) –Harakati ya Kiislamu Nigeria (INM) imesema hatua ya serikali ya nchi hiyo kuendelea kumshikilia Sheikh Ibrahim Zakzaky na mke wake ni ukiukwaji wa wazi wa sharia.

Katika taarifa Jumatatu, INM imesema Mahakama ya Kifiderali Nigeria imesema haki za kikatiba za Sheikh Zakzaky zimekiukwa kutokana na kuendelea kushikiliwa na iliamuru aachiliwe huru.

Wafuasi wa Sheikh Zakzaky wameilani serikali ya Nigeria kwa kukataa kutii amri ya mahakama ya kumuachilia huru mwanazuoni huyo wa Kiislamu.

Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria na mkewe walitiwa nguvuni tarehe 13 Desemba 2015 wakati askari wa jeshi la Nigeria walipovamia na kushambulia Hussainiyah iliyoko katika mji wa Zaria. Katika shambulio hilo, mamia ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Nigeria, wakiwemo wana watatu wa kiume wa Sheikh Zakzaky, waliuawa shahidi.

Baada ya jitihada kubwa, maandamano ya kila pembe na mashinikizo mengi ya ndani na kimataifa, mnamo mwezi Agosti, mahakama ya Nigeria iliruhusu Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe wapelekwe India kutibiwa, lakini kutokana na matatizo na vizuizi vilivyowekwa na maafisa wa usalama walioandamana naye, kiongozi huyo wa kidini pamoja na mkewe waliamua kurudi Nigeria baada ya kukaa India kwa muda wa siku mbili tu pasi na kupatiwa matibabu.

Kabla ya hapo, Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ilikuwa imefichua kwamba, serikali ya nchi hiyo imekula njama ya kumuua Sheikh Zakzaky kwa kutumia mbinu tofauti ikiwemo ya kumpa sumu.

Wfuasi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria wameapa kuendeleza maandamano ya kutaka Sheikh Zakzaky aachiliwe huru.

3470024/

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: