IQNA

Hujuma ya Marekani dhidi ya Hashdu Sha'bi Iraq yaibua hasira na maandamano

16:48 - December 31, 2019
Habari ID: 3472320
TEHRAN (IQNA) - Malefu ya wananchi wenye hasira nchini Iraq leo wameandamana mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Baghdad baada ya mazishi ya wapiganaji wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi maarufu kama Al Hashd al Shaabi ambapo wamelaani vikali hujuma ya anga ya Marekani dhidi ya vituo vya harakati hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa, wananchi wenye hasira wa Iraq wameteketeza moto mlango kati ya milango ya kuingia katika ubalozi wa Marekani mjini Baghdad na kupandaa juu ya ukuta huo ambapo wametundika hapo bendera ya Al Hashd al Shaabi huku wakipiga nara za 'Mauti kwa Marekani'.

Maandamano hayo yamehudhuriwa na Abu Mahdi al Muhandis Naibu Mkuu wa Al Hashd al Shaabi, Qais  Al Khazali kiongozi wa Harakati ya Asa’ib Ahl Al-Haq na Abu Du'aa al-Issawi Naibu wa Masuala ya Jihadi katika Harakati ya Sadr inayoongozwa na Muqatad Sadr.

Kwa mujibu wa taarifa,  baada ya Marekani kushambulia vituo vya Harakati ya Al Hashd al Shaabi na kuibuka maandamano makubwa, balozi wa Marekani mjini Baghdad na wafanyakazi wote wa ubalozi huo wote wametoroka kwa pamoja na hawajulikani waliko.

Hii si mara ya kwanza kwa kambi za wapiganaji hao wa kujitolea wa Iraq kushambuliwa na Wamarekani. Kabla ya hapo, Marekani na washirika wake waliituhumu Hashdu Sha'bi kwa kupora mali, ufisadi wa kimaadili na uchochezi wa kimadhehebu, kutilia shaka mapambano yake dhidi ya magaidi wa Daesh na kuzishambulia kijeshi mara kadhaa kambi zake za kijeshi. Swali linalopaswa kuulizwa ni hili kwamba je, chanzo cha chuki hiyo yote Marekani dhidi ya Hashdu Sha'abi ni nini?

Tunaweza kusema kwamba sababu ya kwanza ya uadui na chuki hiyo ni utambulisho wa Hashdu Sha'abi unaogongana moja kwa moja na wa Marekani. Jeshi la Hashdu Sha'bi ni la wapiganaji wa Kiislamu wa kujitolea nchini Iraq ambalo lina uwezo mkubwa wa kukusanya wapiganaji kwa ajili ya kufikia malengo ya mapambano ya Kiislamu katika eneo. Hii ni katika hali ambayo Marekani ni adui mkubwa wa mapambana kama hayo.

Sababu ya pili  ya uadui wa Marekani dhidi ya Hashdu Sha'bi ya Iraq ni kwa ajili ya kutetea maslahi ya utawala haramu wa Israel. Uwepo na kuimarika kwa wapiganaji hao wa kujitolea wa Kiislamu nchini Iraq kuna maana ya kuimarika ngome ya makundi ya mapambano ya Kiislamu katika eneo, jambo ambalo linagongana moja kwa moja na maslahi ya utawala ghasibu wa Israel, ambao ni mshirika muhimu zaidi wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi. Sababu ya tatu ya uadui wa Marekani dhidi ya Hashdu Sha'bi ni kulizuia kundi hilo la mapambano ya Kiislamu kuingizwa katika muundo mkuu wa utawala wa Iraq. Mbali na Marekani na utawala haramu wa Israel, Saudi Arabia pia ni miongoni mwa wapinzani wakuu wa kundi hilo. Sababu ya Nne ni kwamba Hashdu Sha'bi ina azma thabiti ya kupambana na ugaidi wa Daesh nchini Iraq katika hali ambayo Marekni si tu kwamba haina nia yoyote ya kulifuta kundi hilo la kigaidi bali inafuatilia njia za kuwaingiza tena magaidi hao nchini Iraq kutoka Syria.

3867863

captcha