IQNA

10:39 - January 02, 2020
News ID: 3472326
TEHRAN (IQNA) – Ubalozi wa Marekani mjini Baghdad nchini Iraq, Jumatnao ulitangaza kusitisha huduma zote kwa umma kufuatia maandamano ya wananchi waliokuwa na hasira wa Iraq nje ya ubalozi huo.

Katika kipindi cha siku kadhaa sasa ,wananchi wa Iraq wenye hasira wamkuwa wakikusanyika na kufanya maandamano makubwa mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Baghdad na kuchoma moto milango kadhaa ya ubalozi huo wakijibu na kuonesha hasira yao dhidi ya mashambulizi yaliyofanywa na Marekani katika ngome za harakati ya wapiganaji wa kujitolea ya al Qhashdul Shaabi.

Jumapili iliyopita Marekani ilishambulia ngome na vituo vya harakati ya wananchi wa Iraq ya al Hashdul Shaabi katika eneo la al Qaim mkoani al Anbar na kuua makumi ya wanachama wa harakati hiyo na kujeruhi wengine wengi. Baada ya shambulizi hilo wananchi wa Iraq walifanya maandamano makubwa na kukusanyika mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Baghdad wakitaka kufukuzwa wanajeshi wa nchi hiyo nchini Iraq.

Makundi mbalimbali ya wananchi nchini Iraq yameendelea kutoa wito na kushinikiza kufungwa ubalozi wa Marekani mjini Baghdad.

Jawad al-Talibawi, mmoja wa makamanda wa Harakati ya Wananchi ya al-Hashd al-Sha'abi amesema kuwa, ubalozi wa Marekani mjini Baghdad unapaswa kufungwa kwani ni pango la ujasusi na mahali pa kupangia njama za uharibifu dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Aidha amesema kuwa, matukio yanayotokea mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Baghdad ni radiamali ya kawaida dhidi ya mashambulio ya anga ya hivi karibuni ya Marekani dhidi ya wapiganaji wa al-Hashd al-Sha'bi.

Wakati huo huo, Muhammad Muhyi, msemaji wa Brigedia ya Hizbullah, tawi la kijeshi la Hashd al-Sha'abi amesisitiza juu ya kudumishwa mkusanyiko wa wananchi mbele ya ubalozi wa Mareakni mjini Baghdad hadi ubalozi huuo utakapofungwa.

3868354

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: