IQNA

Kikosi cha Hashdu Shaabi chaangamiza ngome ya ISIS Iraq

21:22 - January 12, 2020
Habari ID: 3472365
TEHRAN (IQNA) - Vikosi vya Kujitolea vya Wananchi wa Iraq maarufu kama Al Hashd al Shaabi vimeharibu pango kubwa zaidi la magaidi wa ISIS (Daesh) kaskazini mwa Iraq.

Kwa mujibu wa taarifa, katika oparesheni hiyo, ghala kubwa la silaha za magaidi wa ISIS limeharibiwa. Shirika la habari la Sumeriya limeripoti kuwa, ghala hilo lilikuwa na vifaa elfu tatu vya kutegea mabomu, maguruneti 100, mishipi 13 ya kujilipua na makombora 30.

Mnamo Januari 3  Al Hashd al Shaabi ilianzisha oparesheni ya kuwatimua magaidi wa ISIS katika eneo la Mosul na pia jana ilianzisha oparesheni nyingine inayojulikana kama Ali Waliullah katika eneo la Al Khadr kwa lengo la kukabiliana na magaidi wa ISIS.

Al Hashd al Shaabi imesema lengo la oparesheni hizo ni kuleta uthabiti katika eneo na kuzuia makundi ya magaidi wakufurishaji kuibuka upya.

Pamoja na kuwa magaidi wa ISIS wametimuliwa katika maeneo yote ya Iraq lakini bado kuna mabaki ya magaidi hao katika maeneo mbali mbali nchini humo na hutekeleza mashambulizi ya kuvizia mara kwa mara.

3871015

captcha