IQNA

18:00 - February 17, 2020
News ID: 3472480
TEHRAN (IQNA)- Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesisitiza kuendelea uungaji mkono wa Iran kwa Syria katika vita dhidi ya ugaidi.

Ali Larijani Jumapili alikutana na kufanya mazungumzo huko Damascus mji mkuu wa Syria na Rais Bashar Assad wa nchi hiyo na kuongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina yakini kwamba Syria inaweza kuwafurusha magaidi katika maeneo yote ya nchi hiyo. 

Katika mazungumzo hayo Rais Bashar al Assad wa Syria pia amekosoa uungaji mkono wa baadhi ya nchi kwa makundi ya kigaidi huko Syria na kueleza kuwa magaidi wamewateka nyara raia huko Idlib kaskazini magharibi mwa nchi hiyo na kuwatumia kama ngao ya binadamu. 

Rais Assad ameashiria hali ya machafuko katika baadhi ya maeneo ya Syria na kusisitiza kuwa Damascus kamwe haitaruhusu kuendelea mchakato huo unaoitishia maisha ya wananchi. Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran Dakta Ali Larijani jana Jumapili aliwasili Damascus mji mkuu wa Syria kwa lengo la kufanya mazungumzo na viongozi wa ngazi ya juu wa nchi hiyo. 

3879407

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: