IQNA

Utawala wa Kizayuni watibu magaidi wa kitakfiri kutoka Syria

13:47 - April 01, 2016
Habari ID: 3470224
Utawala wa Kizayuni wa Israel hadi sasa umetoa matibabu kwa magaidi wa kitakfiri zaidi ya 2,100 wanaopigana ndani ya Syria kuiangusha serikali halali ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA,, duru ndani ya utawala wa Kizayuni zimefichua kuwa Israel ingali inatoa matibabu kwa magaidi wanaOjeruhiwa katika mapigano na vikosi vya Syria na waitifaki wake. Aidha imedokezwa kuwa magaidi hao hasa wa kundi la ISIS au Daesh na wale wa Jabhatu Nusra, tawi la Al Qaeda, wanapata matibabu katika hosptilai za jeshi la Israel katika miinuko ya Golan. Mwezi Juni mwaka 2015 wakaazi Wasyria wa Golan walinasa magari kadhaa ya jeshi la Israel yakisafirisha magaidi wa al Nusra katika eneo hilo. Aidha mwezi Juni mwaka 2014 Kikosi cha Umoja wa Mataifa katika mpaka wa Syria na Israel UNDOF kilifichua kuwa wanajeshi wa Israel wameonekana wakiwasafarisha magaidi kutoka Syria. Kikosi hicho kina jukumu la kusimamia usitishwaji vita wa mwaka 1974 baina ya Israel na Syria. Halikadhalika mwezi Desemba mwaka 2015 kulifichuka video iliyowaonyesha wanajeshi wa Israel wakiwasafirisha kwa gari la kubebea wagonjwa magaidi waliojeruhiwa nchini Syria. Imedokezwa kuwa hadi sasa Israel imetumia dola milioni 13 kuwatibu magaidi kutoka Syria katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Serikali ya Syria inasema nchi za Magharibi na waitifaki wao katika eneo hasa Utawala haramu wa Israel, Saudi Arabia, Qatar na Uturuki ndio waungaji mkono wakuu wa magaidi wanaotaka kuiangusha serikali ya Rais Bashar al-Assad.
captcha