IQNA

18:02 - February 17, 2020
News ID: 3472481
TEHRAN (IQNA) – Kanali ya kwanza ya televisheni ya satalaiti ambayo ni maalumu kwa ajili ya Qur'ani Tukufu imezinduliwa nchini Misri.

Kwa mujibu wa tovuti ya Egypt Independent, kanali hiyo inajulikana kama 'Masr Quran Kareem, inarusha matangazo yake kupitia  Nile Sat Frequency 10853 MHz. Kanali hiyo inalenga kueneza mafundisho ya Qur'ani sambamba na kuhuisha qiraa (usomaji) ya Qur'ani ya Wamisri ambayo ni mashuhuri duniani.

Msemaji wa shirika la huduma za vyombo vya habari la United Group Hossam Saleh amesema qiraa nadra za wasomaji maarufu wa Qur'ani Misri zitarushwa hewani katika kanali hiyo. Miongoni mwa qiraa zitakazorushwa hewani ni za  Said al-Naqshbandy, Mohamad Siddik al-Minshawy, Abdul Baset Abdul Samad, Mohamad Rifaat na Mahmoud Ali al-Banna. Amesema kwa sasa kanali hiyo imeanza kwa majaribio na ratiba kamili ya matangazo itatangazwa baadaye.

3470656

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: