Makundi hayo ya kupigania ukombozi Palestina yamesisitiza kuwa, matokeo hayo ya uchaguzi yanayonyesha kuwa utawala wa Kizayuni unakusudia kuendeleza sera zake za ubaguzi na apatheidi dhidi ya watu wa Palestina.
Katika taarifa, Fauzi Barhoum, Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina amesema, mapambano ya kupigania ukombozi wa Palestina yataendelea bila kujali ni serikali gani inayochukua madaraka Israel.
Naye Dawud Shahab mmoja kati ya makamanda wa Harakati ya Jihad Islami amesema matokeo ya uchaguzi wa bunge la Israel hayabadilisho ukweli wowote kwani ardhi za Palestina zinaendelea kukaliwa kwa mabavu na hivyo mapambano yanapaswa kuendelea dhidi ya Wazayuni maghasibu. Naye Mustafa Al Bargouthi, Katibu Mkuu wa Harakati ya Ubunifu wa Kitaifa Palestina anasema matokeo ya uchaguzi wa bunge la Israel yanaonyesha kupata uungaji mkono wanasisia wabaguzi na wenye misimamo mikali. Ameongeza kuwa nukta hiyo inaonyesha kuwa jamii ya Israel inaunga mkono ubaguzi na mfumo wa apatheidi katika utawala huo bandia.