Kwa mujibu wa taarifa, Idara ya Wakfu ya Mji wa Quds imetangaza kuwa: "Baada ya kila sala Msikiti wa Al-Aqsa unanyunyiziwa dawa ya kuua virusi vya Corona ili kuzuia ugonjwa huo kuenea miongoni mwa waumini wanaofika hapa kuswali."
Taarifa hiyo imeoneza kuwa, kufuatia ushauri wa Wizara ya Afya ya Palestina, oparesheni ya kunyunyizia dawa ya kuua virusi katika Msikiti wa Al Aqsa ilianza Alhamisi. Aidha anasame dawa inayotumiwa imeidhinishwa na Wizara ya Afya ya Palestina na Shirika la Afya Duniani na hivyo haina madhara kwa mwanadamu.