IQNA

12:50 - March 18, 2020
News ID: 3472579
TEHRAN (IQNA) – Baadhi ya misikiti katika mji wa Cape Town Afrika Kusini imetangaza kufunga milango yake kwa muda ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19 au corona.

Imamu wa msikiti wa Masjidul Quds mjini Cape Town, Sheikh Abdulrahman Alexzander amesema msikiti huo unafundw akwa muda kuanzia Jumanne.

"Kwa niaba ya uongozi wa msikiti, tunasikitika kutangaza uamuzi kuwa Masjidul Quds mjini Cape Town itafungwa kuanzia Jumanne asubuhi 17 Machi 2020," amesema Imamu wa msikiti Jumatatu kwa njia ya video akiwa ameandamana na maafisa wa msikiti huo. Amesema kufuatia kufungwa msikiti, sala za jamaa za kila siku hazitaswaliwa kama ambavyo pia hakutakuwa na sala za Ijumaa. Sheikh Alexander amesema uamuzi huo umekuja baada ya mashauriano ya kina kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa baada rais Cyril Ramaphosa kutangaza amri ya kupiga marufuku mjumuiko wa zaidi ya watu 100 eneo moja ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.

Mnamo Machi 15 Rais Ramaphosa alitangaza hali ya hatari kitaifa ili kukabiliana na kirusi cha corona ambacho hadi sasa kimewasibu watu 62 nchini humo. Misikiti mingine ambayo imefungwa kwa muda Cape Town ni pamoja na Msikiti wa Claremont na Msikiti wa Shukrul Mubeen eneo la Lansdowne.

3470950

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: