IQNA

10:36 - March 26, 2020
News ID: 3472602
TEHRAN (IQNA)- Wananchi wa Mauritania wamerejea kwenye Qur'ani Tukufu kwa ajili ya kuomba uponyaji au shufaa na maombezi na kuweza kushinda mashinikizo ya kiakili na kinafsi yanayosababishwa na hofu ya maambukizi ya kirusi cha corona kinachoendelea kusambaa kwa kasi kubwa katika nchi mbalimbali duniani.

 Yaslam al Maqari ambaye ni Mshauri wa Wizara ya Masuala ya Kiislamu nchini Mauritania ameandika katika ukurasa wake wa Twitter na Facebook kwamba: Wizara hiyo imewataka wasimamizi wa misikiti yote nchini kurusha hewani qiraa na visomo vya Qur'ani tukufu kupitia vipaza sauti vya misikiti.

Baada ya watu kadhaa kupatwa na virusi vya corona nchini Mauritania, serikali ya nchi hiyo imechukua hatua kadhaa za kukabiliana na janga hilo ikiwa ni pamoja na kufunga shule, kupiga marufuku safari za anga na kufunga baadhi ya mipaka ya nchi hiyo.

Idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa ugonjwa wa COVID-19 au corona kote barani Afrika imepindukia watu 1,114 katika nchi 40 barani humo. 

Hadi kufikia Jumamosi iliyopita nchi za Misri, Afrika kusini na Algeria zilikuwa zikiongza kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya virusi vya corona.

3887010

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: