IQNA

Sisitizo la kufundishwa watoto Qur’ani katika chekechea nchini Mauritania

14:46 - September 10, 2020
Habari ID: 3473155
TEHRAN (IQNA) – Mbunge mmoja nchini Mauritania ameitaka serikali ya nchi hiyo kuhakikisha kuwa Qur’ani Tukufu inafunzwa katika chekechea zote nchini humo.

Ould Al Khalifa, mjumbe katika Bunge la Mauritani amesema ili jamii iweze kusatawi katika Nyanja zote na iwe na wanaadamu wanaofahamu sifa za mwanadamu, kuna haja ya kuwepo mafunzo ya Qur’ani katika chekechea zote nchini humo. Aidha amesema mafunzo ya Qur’ani yanapaswa kuwa kwa mujibu wa mpango na mataala maalumu ambayo utatayarishwa kwa ushirikiano wa Wasomi wa Uislamu na waalimu.

Akizungumza katika kikao cha bunge cha kuchunguza baraza la mawaziri walioteuliwa na Waziri Mkuu Mohamed Ould Bilal, Al Khalifa amesema bunge linaunga mkono mafunzo ya Qur’ani katika vituo vyote vya elimu nchini humo huku akisisitiza kuwa, kulipata taifa mafunzo ya Qur’ani kutaibia jamii yenye kufuata njia ya haki, yenye utulivu, uadilifu na maelewano.

Aidha mbunge hiyo ameanzisha kampeni ya kuwepo mafunzo ya Qur’ani kwa njia ya intaneti katika kipindi hiki cha janga la corona.

3922007

captcha