IQNA

Kampeni ya qiraa ya Qur’ani Mauritania wakati wa janga la COVID-19

20:33 - December 13, 2020
Habari ID: 3473452
TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Mauritania imeendeleza kampeni maalumu ya qiraa ya Qur’ani katika misikiti ya nchi hiyo.

Wizara hiyo imetoa agizo kwa maimamu wote wa misikiti nchini humo kuweka kanda za qiraa ya Qur’ani nyakati mbali mbali katika kipindi hiki cha janga la COVID-19  nchini humo.

Mpango huo unalenga kuwasaidia waumini kimaanawi katika siku hizi ngumu za janga la COVID-19.

“Tutaangaiza COVID-19 kwa msaada wa Qur’ani Tukufu” ni nara na kauli mbiu ya kampeni hiyo.

Nchi hiyo ya kaskazini magharibi mwa Afrika inakabiliwa na wimbi la pili la maambukizi ya corona au COVID-19.

Hadi sasa watu zaidi ya 11,000 wameambukizwa corona nchini humo huku wengine 222 wakipoteza maisha.

Mauritania ni Jamhuri ya Kiislamu na ina idadi ya watu milioni nne ambao karibu wote ni Waislamu.

3940785

captcha