IQNA

Wamauritania wafurahi baada ya misikiti kufunguliwa - Video

12:37 - May 11, 2020
Habari ID: 3472756
TEHRAN (IQNA) – Baada ya Mauritania kuondoa vizingiti vilivyokuwa vimewekwa ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19, misikiti imefunguliwa nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa, baada ya misikiti kufunguliwa,  mamia ya waumini waliweza kufika katika msikiti mkubwa zaidi katika mji mkuu wa Mauritania, Nouakchott kwa ajili ya Swala ya Ijumaa.

Jumatano iliyopita Mauritania ilitangaa kufunguliwa tena maeneo ya umaa baada ya kufungwa kwa miezi miwili, Kati ya maeneo yaliyofunguliwa ni masoko ya kale, migahawa na misikiti. Wananchi wametakiwa wazingatia kanuni za kiafya kuhusu COVID-19 ili kuzuia kuenea ugonjwa huo hatari.  Kati ya kanuni ambazo ni lazima kutekelezwa  ni uvaaji maski au barakoa, watu kutokaribiana na kunawa mikono. Tizama video hapa chini

3897736

 

captcha